Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

WIZARA YA AFYA YAFANYA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA HUDUMA ZA UTENGAMAO, TIBA SHUFAA NA HUDUMA ZA USIKIVU

Posted on: December 10th, 2024

Timu ya Usimamizi Shirikikishi katika huduma za Utengamao, Tiba Shufaa, Sikio pua na koo kutoka Wizara ya Afya imefanya Ukaguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe leo Desemba 11, na kupokelewa na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe akiwemo Kaimu Mganga Mfawidhi, Dkt. Rasuli Chihako, Katibu wa Afya, Bi. Tekla Myumbilwa, na Mratibu wa Uhakiki wa Ubora wa Huduma kwa Mteja, Ashery Mwalukolo.

Pamoja na kupongeza Uongozi wa Hospitali na watumishi kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, wameshauri Hospitali iboreshe mikakati ya kuongeza wataalamu katika huduma za utengamao na huduma za Masikio, Pua na Koo.

Kaimu Mganga Mfawidhi ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma za afya ikiwepo kuajiri watumishi katika idara za utengamao pia ameomba nguvu zaidi iongezwe kwenye maeneo hayo ili kuboresha utolewaji wa huduma hizo