Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

MAFUNZO YA HUDUMA BORA KWA MTEJA

Posted on: November 23rd, 2021

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe walishiriki mafunzo ya huduma bora kwa mteja yaliyofanyika kuanzia tarehe 15 Novemba 2021 hadi tamati yake mnamo tarehe 18 Novemba 2021. mafunzo haya yalilenga mabadiliko chanya kwa watumishi na jitihada zaidi katika kuhakikisha tunaendelea kuboresha huduma kwa mteja Hospitalini. Aidha mganga mfawidhi Dkt Winfred Kyambile aliwataka watumishi wote wahudhurie mafunzo hayo bila kukosa, kwani kutoa Huduma bora kwa mteja ndio kipaumbele cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.