Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

DKT. MHINA AWAKARIBISHA WENYE CHANGAMOTO ZA UZAZI

Posted on: January 6th, 2025

Wananchi wa Mkoa wa Njombe wamehamasishwa kuendelea kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kunufaika na Huduma za Kibingwa zinazotolewa kila siku.

 Wito huo umetolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Edward Mhina, ambaye amerejea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe baada ya kuwa masomoni kwa Miaka mitatu.

 Dkt. Mhina anafanya hesabu ya kuwa na Madaktari Bingwa wa Mgonjwa ya Wanawake na Uzazi kufikia watatu, Njombe RRH, akiwemo Dkt. Richard Machange, na Dkt. Mafwiri. 

Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwezesha wataalamu mbalimbali kujiendeleza katika Ubingwa na Ubingwa Bobezi, huku akipongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe. 

Mwingine aliyerejea kutoka Masomoni ni Dkt. George Mkumbi ambaye alikuwa akijiendeleza katika Ubingwa wa Magonjwa ya Ndani yanayo jumuisha Shinikizo la Damu, Magonjwa ya Moyo na Figo. 

Madaktari bingwa hawa wanaungana na madaktari bingwa wengine waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Njombe katika nyanja mbalimbali ikiwemo; Upasuaji wa jumla, Upasuaji wa mifupa, Magonjwa ya watoto, Wagonjwa mahututi, ganzi na usingizi, Upasuaji wa Mifupa, Ubingwa kwa Magonjwa ya Watoto, Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, na Magonjwa ya ndani.