Contact Us | FAQ | Mails | Complaints |

FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA

Posted on: March 10th, 2020

VIRUSI VYA CORONA NI NINI?

Kuna vimelea vingi vya magonjwa duniani kote kama Bakteria , Virusi ,Fangi ,Protozoa na Parasaiti

Aghalabu katika makundi yote haya Kuna aina za vimelea ambavyo huwa hatarishi mno na huua haraka wanyama wanyonyeshao na ndege (ambayo ndio makundi yanayoathiriwa mno na vimelea hivi)

Milipuko ya tauni ,kipindupindu(cholera) ,ebola ,malaria Homa ya ini (hasa hepatitis B ) ,Ukimwi (HIV) na homa za mafua vimekuwa tishio kwa miaka mingi nyuma na hivi karibuni na kuua watu wengi mno.

Barani Afrika bado tunao upungufu mkubwa was kupata taarifa za kutosha kuhusu mazingira ,mwingiliano wa viumbe hai na Afya kwa ujumla.

Jamii kubwa barani Afrika na nchi nyinginezo za ulimwengu wa tatu ni jamii ya watu wenye Elimu ya chini mno kuweza kuelewa kwa undani taarifa hizi na na hivyo kupelekea kuathirika mno na magonjwa.

Kuna makundi mengi mno ya virusi duniani kote ,na mengi ya makundi hayo hayana tiba maalumu japo Kuna maendeleo makubwa ya utengenezaji na uboreshaji wa chanjo ,madawa ya kupunguza makali ya maambukizi na kuzaliana pamoja mbinu mbalimbali za kujikinga.

mambo machache kuhusu virusi vya Corona .Ambavyo pia vina makundi manne ya alpha,beta,gamma na Delta 

Jina *"coronavirus"* limetokana na neno la Kilatini na *κορώνη* au *korṓnē,* ikimaanisha *taji* (neno la kiingerza *Crown*

Hii NI kwa sababu ya muonekano wa tabia wa umbo la kirusi hiki ukitumia darubini ya elektroni, ambayo itakuonyesha umbo kama la *taji ya kifalme* au alama ya jua.

Watu mamia kwa mamia wanazidi kufa huko China na historia ya Muda mrefu ya mlipuko wa virusi vya corona huko mashariki ya kati.

Virusi vya Corona ni kundi la virusi ambavyo husababisha magonjwa katika mamalia na ndege.

Kwa wanadamu, virusi hivi husababisha magonjwa ya kupumua ambayo kitaalamu huitwa Systemic Acute Respiratory Syndromes (SARS) aina mojawapo ya Pneumonia ambayo kwa kawaida hupelekea mgonjwa kupumua kwa shida sana na kukosa nguvu , kukohoa na homa Kali Coronaviruses husababisha homa Kali na uvimbe katika koo, kwa wanadamu hasa wakati wa msimu wa baridi.

Coronaviruses wanaaminika kusababisha asilimia kubwa ya homa zote za kawaida kwa watu wazima na watoto.

Virusi hivi vina protini zinazoweza kuvisaidia kushikilia na kuishi kwa kutegemea seli za viumbe hai wengine na gamba maalumu linaloathiri kemikali/enzyme za Figo na kupelekea kuharibika haraka kwa Figo na viungo vingine hasa kwa wagonjwa wenye Kinga ndogo ya mwili.

SARS huweza kupona ndani ya kipindi kifupi ,lakini Muda mwingine yanaweza kuwa mabaya na kupelekea kifo.

Katika ng'ombe na nguruwe (Feline Coronavirus)zinaweza kusababisha kuhara, wakati katika kuku zinaweza kusababisha ugonjwa wa kupumua kwa shida

Maambukizi ya Corona yaliiyotangazwa sana ya binadamu baada ya kugunduliwa ni Yale ya mnamo mwaka 2003, SARS-CoV2003

Maambukizi haya ya tofauti husababisha mkusanyiko wa magonjwa ya kupumua kwa shida na ni ya kipekee kwani hupelekea matatizo ya kupumua ya juu kwenye koo la hewa na ya chini kwenye mapafu

Mpaka Sasa Kuna aina saba za Corona wanaathiri binadamu 

  • Human Coronavirus 229E (HCoV-229E)
  • Human Coronavirus OC43 (HCoV-OC43)
  • SARS-CoV
  • Human Coronavirus NL63 (HCoV-NL63, coronavirus mpya ya Haven huko )
  • Human Coronavirus HKU1
  • Middle East Respiratory syndrome Coronavirus MERS-Cov
  • Novel coronavirus (2019-nCoV)


Novel coronavirus (2019-nCoV)

inajulikana pia kama *Wuhan pneumonia* au Wuhan coronavirus kwa sababu imegunduliwa katika Jimbo la Wuhan huko China na kutambuliwa na mamlaka huko Wuhan, Hubei, Uchina, kama sababu ya mlipuko wa coronavirus unaoendelea wa 2019-20.

Jina hili linatokana na ugunduzi mpya, na Imegunduliwa karibuni tu Disemba mwaka jana na ndio imekuwa tishio mpaka Sasa huko china.

Novel Coronavirus ya 2019 (2019-nCoV) ni virusi vya kuambukiza ambavyo husababisha maambukizo ya kupumua na tayari tafiti zimeonyesha ushahidi wa maambukizi kati ya Mtu na mtu kama ilivyothibitishwa huko Guangdong, china, Januari 20, 2020.

Kuna ripoti ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba maambukizi haya kutokea kwa vyakula wa baharini ,nyoka na popo ambayo ni vyakula vya kitamaduni vya kichina na tafiti nyingi zinaonesha Coronavirus kuishi ndani ya viumbe hawa pia. Virusi hivi pia hukaa ndani ya paka ,nguruwe na hata ngamia.

Ulinganishoo wa maumbile kati ya virusi hivi na sampuli zingine za virusi zilizopo zimeonyesha kufanana kwa SARS-CoV (79.5%)

Mlipuko wa kwanza Virusi umegunduliwa huko Wuhan, Uchina, katikati ya Desemba 2019 na baadaye vilienea kwa kasi katika majimbo mengine ya Bara la China na nchi zingine, pamoja na Thailand, Japan, Taiwan, Korea Kusini, Australia, Ufaransa, na Amerika.

Kufikia tarehe 27 Januari 2020, tayari kuna kesi 2,006 zilizothibitishwa za maambukizi ambapo 1825 wako ndani ya China Bara. Idadi ya vifo mpaka Sasa imefikia 81 kutoka tar 27 Januari 2020.

kuenea kwake

Coronavirus ni ugojwa unaoambukiwa Kwanza kutoka kwa wanyama au kwa kitaalamu huitwa ZOONOSTIC INFECTIONS na mtu aliyeambukizwa huweza kueneza kwa wengine kwa njia ya hewa pale akikohoa ,kupumua au kupiga chafya. 

Dalili 

Kuna dalili kuu nne za awali ambazo ni

  • Uchovu,
  • kikohozi kikavu,
  • upungufu wa pumzi, na
  • shida ya kupumua.

Kesi za maambukizo mazito zinaweza kupelekea pneumonia, kuharibika kwa figo, na hata kifo. Katika taarifa iliyotolewa tarehe 23 Januari 2020, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom alisema kwamba robo ya wale walioambukizwa walipatwa ghafula na kwamba wengi wa wale waliokufa walikuwa na hali zingine kama shinikizo la damu, ugonjwa wa sukari au ugonjwa wa moyo na mishipa ambayo ilisababisha kinga yao kuwa chini kuweza kupambana na maambuki haya.

Utafiti wa wagonjwa 41 wa kwanza waliolazwa katika hospitali za Wuhan na kesi zilizothibitishwa ziliripoti kuwa wagonjwa wengi walikuwa na afya kabla ya kuambukizwa ugonjwa huo, na kwamba zaidi ya robo ya watu wazima wenye afya walihitaji huduma ya uangalizi wa karibu. Kati ya idadi kubwa ya wale walielazwa hospitalini, walikuwa na idadi ndogo ya seli nyeupe za damu na kiwango cha chini cha damu.

Matibabu .

Mpaka Sasa Hakuna matibabu maalumu ya Coronaviruses zaidi ya kutibu dalili na matatizo yasabishwayo na Virusi hawa kama Homa ,maumivu ya viungo ,hewa ya oksijeni na dawa za kusaidia upumuaji .

Kuna tafiti nyingi bado zinaendelea mpaka sasa.